Na Majid Ahmed, Mogadishu
Mwaka mmoja wa kulegezwa kwa kikwazo cha silaha kwa Somalia na Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kutaiwezesha serikali kununua silaha
nyepesi nyepesi kwa ajili ya vita vyake dhidi ya al-Shabaab, lakini
baadhi ya wachambuzi wanaonya kuwa kwa kufunguliwa kwa njia ya silaha
kunaweza kuruhusu silaha kuishia katika mikono isiyotakiwa.
Chini ya Azimio 2093 la Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa, Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM)
itaendelea kubakia huko hadi mwezi Februari 2014. [Na Stuart Price/AU-UN
IST/AFP]
Azimio nambari 2093 linairuhusu Somalia kununua silaha zenye ukubwa wa
mwisho wa kipenyo cha milimita 12.7. Azimio pia linarefusha mamlaka ya
jeshi la askari 17,000 la Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia
(AMISOM) hadi tarehe 28 Februari, 2014.
Katika azimio hilo, serikali ya Somalia lazima itoe siku tano za taarifa
kwa kamati inayoshughulikia na usimamizi wa vikwazo vilivyowekwa na
Umoja wa Mataifa kuhusu uingiaji wa shehena wa silaha nyepesi. Somali
pia lazima itoe ripoti kila baada ya miezi sita juu ya mpango wake wa
kuhakikisha utunzaji salama wa silaha hizo.
Ulinzi
Mwanachama wa Brigedi ya Ras Kamboni
ambayo inaiunga mkono serikali akinyanyua bunduki nzito aina ya mashine
akiwa amepanda nyuma ya gari ya mzigo huko Kismayo mwezi Oktoba 2012.
[Na Stuart Price/AU-UN IST/AFP]
"Hatua hii ya kulegeza kikwazo cha silaha kilichowekewa Somalia ni
mafanikio makubwa kwa watu na serikali ya Somalia, na inaonyesha hatua
chanya katika kipengele cha imani ya jumuiya ya kimataifa kwa serikali
mpya ya Somalia," alisema Waziri wa Ulinzi wa Somalia Abdihakim Haji
Mohamud Fiqi.
Fiqi alisisitiza kuwa kulegezwa kwa kikwazo kutaisaidia serikali ya
Somalia kutimiza lengo lake kuu la kuwavunjavunja al-Shabaab. "Kwa vile
sasa kikwazo kimelegezwa, serikali ya Somalia inayo nafasi ya kununua
silaha nyepesi kwa dhamiri ya kuimarisha usalama wa vikosi vyake na
kuviwezesha kufanya kazi zao za ulinzi kwa ufanisi zaidi," aliiambia
Sabahi.
Comments