Waasi wa M 23 |
Na Victor Melkizedeck Abuso
Serikali ya Rwanda kupitia Waziri wa mambo ya nje Louise Mushikiwabo
imetupilia mbali madai ya serikali ya DRC kuwa Jenerali Bosco Ntaganda
anayesakwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivta ICC amevuka
mpaka na kuingia Rwanda.
Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa juma lililopita, wapiganaji wapatao 700 wa
M 23 wa upande wa Jean- Marie Runiga walivuka mpaka kukimbilia nchini
Rwanda baada ya makabiliano makali na upande wa M23 wanaoongozwa na
Sultan Makenga.
Hata hivyo, serikali ya DRC kupitia msemaji wake Lambert Mende inaomba
nchi ya Rwanda kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria vya kimataifa wale
ambao wanatafutwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita.
Mashirika ya kiraia katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini kwa upande wao,
yametoa msimamo wao kuhusiana na taarifa hizo, huku Omar Kavota naibu
Mwenyekiti na msemaji wa mashirika hayo akisema viongozi hao wa M 23
wameitwa Rwanda na viongozi wa serikali hiyo.
Comments