Na Bashir Nkoromo
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka
nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya
kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha
nchi hiyo.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana |
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) , Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro amesema leo kwamba katika ziara hiyo
Kinana atakuwa na msafara wa watu 14, ambao baadhi yao ni Wajumbe wa
Kamati kuu ya CCM, Makatibu wakuu wa Jumuia za Chama na Wenyeviti wa
Chama wa mikoa.
Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es
Salaam, Dk. Asha-Rose alisema, Kinana na msafara wake wanatarajiwa
kufika Guangzhou China keshokutwa, Machi 12, 2012.
Alisema, ziara hiyo ambayo ni ya kwanza nje ya nchi kwa Kinana tangu
kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba, mwaka jana,
imeandaliwa na Chama Cha Kimomunisti cha China kwa lengo la kupata fursa
ya viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo kubadilishana uzoefu katika
nyanja mbalimbali za kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya vyama na
wananchi wa nchi Dk. Asha-Rose alisema baada ya kuwasili Guangzhou,
kinana na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao wa Chama Cha Kikomunisti cha
China watatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo jiji la Dong-guan,
Shenchen, Chengdu, Machi 13-14, 2013, msafara utakwenda jiji la Chengdu,
Sichuan, Nanchong na kumalizia ziara hiyo katika jiji la Beijing ambako
atawasili Machi 18, 2013.
Comments