KATIKA Jukwaa la Sanaa Jumatatu ijayo ya Tarehe 23, Agosti, 2010, Jopo la Wataalam Kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) litafafanua na kuwajengea kichwani Wasanii na wadau wote wa sanaa elimu na mkakati kapambe wa Kurasimisha Sekta ya Sanaa Nchini.
Lengo ni kurasimisha Rasilimali na Biashara za Sanaa nchini ili kuwapa hadhi wasanii na wadau wa sanaa, kuwawezesha kukopesheka kwenye taasisi za kifedha, kuwafungulia mianya ya kibiashara na kikazi,kuwapa fursa ya kuongeza pato binafsi na lile la Taifa, kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, kubana makanjanja kwenye fani ya sanaa,kuwaandaa wadau kwa ajili ya soko la pamoja la Afrika Mashariki na masuala mengine kibao.
Wasanii na Wadau wa Sanaa hawana budi kuja kwa wingi Kuanzia saa 4 Asubuhi kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba (Shuka Ilala,Bungoni kisha ulizia ilipo BASATA au Chuo cha DSJ) ili kufaidi mwanya huo na Jopo la Wataalamu Kutoka MKURABITA.
Comments