NEWYORK,Marekani
BINTI wa nyota wa zamani wa Pop Michael Jackson,Paris ameripotiwa kumfukuza kazi msaidizi wa nyumba hiyo wa siku nyingi, Grace Rwaramba baada ya mfululizo wa visa ndani ya nyumba yao.
Jarida hilo liliripoti kuwa mtoto huyo wa mfalme wa zamani wa Pop anadai kutofurahishwa na mtumishi huyo wa ndani baada ya kufanya mahojiano na kituo cha televisheni kuhusu tabia ya marehemu baba yake kuhusu matumizi ya dawa na fedha zake.
"Hatumtaki na hatutaki aishi mahali hapa,"alisema Paris.
Hadi anafukuzwa kazi, Rwaramba amefanya kazi katika familia ya Jackson kwa kipindi cha miaka 17 na amekuwa akihusishwa na masuala mbalimbali na dada yake Michael, Rebbie na watumishi wengine ndani ya nyumba.
Comments