KURA za maoni zanzibar, wengi wasema NDIYO kutaka serikali ya mseto
Registered Voters - 407,669Valid Votes - 266,064Invalid Votes - 8,309Total Turn Out - 274,373Percent Turn Out - 67.00%Polling Stations Published 1,210 of 1,292NDIO / YES = 175,476HAPANA / NO = 90,588Kura za maoni katika Visiwa vya Zanzibar yanafanya kuwapo na muundo mpya wa serikali katika viswa hivyo baada ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na idara ya Maelezo Zanzibar zinaonyesha kwamba asilimia 66.4 ya Wananchi waliopiga kura wameridhia serikali ya mseto, yaani Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Matokeo hayo sasa yanaashiria kuzikwa kwa mfumo wa “Westminster” wa anayeshinda kuunda Serikali kwa kuchukua kila kitu, sasa kazi iliyobaki ni kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitisha mabadiliko ya Katiba Agosti 9 mwaka huu ili kuwapo kikatiba mfumo mpya wa muundo wa Serikali ya Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Khatib Mwinchande alisema waliochagua ndio wameshinda kwa kura 188,705 ikiwa ni sawa na asilimia 66.4 wakati waliochagua hapana wamepata kura 95,613 ikiwa sawa na asilimia 33.6. Mwenyekiti huyo alisema idadi ya kura zote ni 293,339 sawa na asilimia 71 wakati waliojiandikisha ni 407,669.
Kisiwani Pemba wananchi wengi wa huko wamechagua ndio wakati Mkoa wa ya Kusini Unguja kuna idadi kubwa ya watu waliochagua hapana.21,394 sawa na asilimia 66.3 waliochagua ndio 10,864 sawa na asilimia 33.7 katika Mkoa huo, kura zilizoharibika ni 934 ikiwa ni asilimia 2.8%. kura zote ni 33,192 ikiwa sawa na asilimia 69.1.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) Seif Shariff Hamad alisema “Nimefurahishwa namatokeo ya kura ya maoni zilizopigwa na wananchi wa Zanzibar, ni matokeo yao yanayoonesha hisia za demokrasia”Taarifa nyingine toka mitaani zinasema kuwa majimbo yaliyoshikilia kura ya HAPANA ni Amani, Chaani, Chwaka, Dole, Kwahani, Makunduchi, Muyuni na Uzini.

Comments