Skip to main content

MATUKIO NA HABARI ZA KIPOLISI JIJINI DAR ES SALAAM

WATU watatu wamelipotiwa kufa katika matukio tofauti yaliyotokea juzi jijini Dar es Salaam likiwemoo la mwanamke wa (75) kujinyonga kwa kutumia mtandio
Akiongea na waandishi wa Habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema tukio la kujinyonga lilitokea jana majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko Kitunda Machimbo, mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Paulina Nyambega(75) akiwa bafuni amejinyonga kwa kutumia mtandio aliyoutundika kwenye dali la bufu hiyo.
Aidha inadaiwa marehemu alifika nyumbani hapo kwa mkwewe Christine Julius(33) akitokea Tarime miezi miwili iliyopita, hata hivyo awali inadaiwa marehemu aliwahi kutamka kua amebakiza siku chache za kuishi hivyo anataka kugawa urithi kwa watoto wake wote.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Amana na sababu za kupelekea kujinyonga hazijafahamika.
Katika tukio jingine, Kamanda Shilogile alisema gari aina la Fuso namba T433ABY aina ya Benz Truck lilimkanyaga kichwa mzoa takataka na kusababisha kifo chake papo hapo.
Akielezea ajali hiyo, Shilogile alisema kua tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, wakati gari hilo linafanya shughuli za kubeba takataka Manispaa ya Ilala, likiendeshwa na Moses Peter(38) lilipofika barabara ya Morogoro kuelekea Kigogo Sambusa, ghafla mtu mmoja mwanaume ambaye bado hajafahamika kwa jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka (20-25) alidondoka chini ya tairi na kukanyagwa kichwa na matairi ya gari hilo na kupelekea kifo chake.
Shilogile alisema kua marehemu alivaa kaptula ya jinsi,fulana nyeusi na raba nyeupe, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na dereva amekamatwa.

Mbali na tukio hilo, Kamanda Shilogile alisema mpita njia mwamke aliyefahamika kwa jina la Honolinda Kimbavala (49), alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari aina ya Scania yenye namba T 567 ACE, iliyokua na trela namba T 227 ABU iliyokua ikiendeshwa na Thomas Isack (26).
Shilogile alisema kua ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu asubuhi katika barabara ya Nyerere eneo la Tazara, Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Temeke na dereva amekamatwa. Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja aliokotwa akiwa ndani ya mfuko wa kaki huko maeneo ya Kigamboni magongoni akiwa ametupwa na mwanamke asiyejulikana.
Akiongea na waandishi wa habari, Kamamnda wa Polisi mkoa wa Temeke David Msiime alisema kua tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nne na nusu asubuhi, kichanga hicho kiliokotwa na wapiti njia.

Kamanda Msiime alisema kichanga hicho kimehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili na hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri.
Upelelezi wa kumsaka mwanamke aliyefanya tukio hilo unaendelea.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...