Michuano ya Kombe la Dunia , zilianza jana kwa wenyeji Afrika Kusini kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mexico, katika mechi ya Kundi A iliyopigwa katika Uwanja wa City Soccer wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 94,700 mjini hapa.
Mshambuliaji Siphiwe Tshabalala aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli la kwanza la michuano hiyo kwa Bafana Bafana katika fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010.
Mchezaji huyo alifunga goli hilo dakika ya 55, lakini matumaini yao ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo, yalikatishwa na Mexico ambayo ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Rafael Marquez, zikiwa zimesalia dakika 11 mpira kuisha.
Hapa JIJINI Dar es Salaam kulionekana mashabiki wengi kujongea sehemu zenye kuonesha mpira , katika maeneo mengi kama baa na sehemu nyingine kemkem , timu ya Mexico ambayo ilitawala kipindi cha kwanza na ilikosa nafasi nyinngi hadi, Tshabalala alipopata pasi nzuri ya Teko Modise na kumfunga kipa wa Mexico, Oscar Perez katika dakika ya 55.
Tangu nianze kuona michuano hii kiuhalisia nikiwa kijana wa miaka takribani Saba hivi jijini Mwanza ambapo eneo kama la Communitt Center katika kata ya Mirongo nahakika michuano hii naiona kuwa ya kivutio kikubwa kama nilivyokuwa nimeona mechi mbali mbali miaka ya tisini kuja juu kwani watu mbali mbali wanaonekana kufuatilia michuano hii kwa umakini nalejea tena.
Wakicheza mbele ya mashabiki 90,000, ndani ya uwanja wa wao Soccer City, Bafana bafana hawakuweza kuibuka na ushindi.
Kipindi cha pili Bafana Bafana ikiwa katika jitihada za kuongeza mashambulizi, ilijisahau ambapo kiungo wa Mexico, Marquez aliinasa vizuri pasi ya Andres Guardado na kufunga goli la kusawazisha.
Timu zote zilicheza kwa nguvu kutaka kupata goli la ushindi na Katlego Mphela, angeweza kufunga goli la ushindi dakika 85 wakati alipopiga shuti na mpira kugonga mlingoti wa goli na kurudi uwanjani.
Awali Mexico ilifunga goli dakika ya 38, lililofungwa na Carlos Vela lakini lilikataliwa na mshika kibendera kwa madai kuwa mfungaji akulikuwa ameotea wakati beki mmoja Bafana Bafana alikuwa kwenye mstari wa goli pamoja na kipa ambaye alitoka.
Afrika Kusini inayonolewa na Carlos Perreira, ilijibu shambulizi dakika ya 44 ambapo, Tshabalala aliunganisha mpira wa kona na kipa Perez aliupangua na kuwa kona nyingine.
Mechi hiyo ilitanguliwa na sherehe za ufunguzi wa mashindano zilizoongozwa na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliyefungua rasmi mashindano hayo, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter aliyetoa iliyeipongeza Afrika Kusini kwa maandalizi mazuri.

Comments