Skip to main content

Wanne C.C.M Kugombea Jimbo la Kwele

BAADA ya Mbunge wa jimbo la Kwela Sumbawanga Vijijini, Dk.Chrisant Mzindakaya, kutangaza kwamba hana mpango wa kugombea ubunge mwaka huu, wanachama wanne wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuwania nafasi hiyo akiwemo Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji kilichopo jijiji Mbeya, Stephen Chambanenge.Chambanenge ambaye yupo kwenye kitivo cha Sayansi ya Jamii katika chuo hicho,akizungumza na Nipashe jana alisema ameamua kugombea ili kuleta changamoto mpya ya maendeleo katika jimbo hilo ambalo linakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ubovu wa miundombinu hususani ya barabara."Ubunge wa sasa unahitaji mtazamo mpya unaoshabihiana na kasi ya karne ya Sayansi na Teknolojia hivyo maarifa ya kisasa na uwezo wa kufikiri na kutenda kwa haraka kunahitajika ili kuleta kasi ya maendeleo,"alisema Chambanenge.Alisema jimbo la Kwela ambalo asilimia zaidi 80 ya wakazi wake ni wakulima bado linakabiliwa na matatizo kadhaa kama vile ukosefu wa soko la uhakika la kuuzia mazao yao na hivyo wafanyabiashara wakubwa kuwalangua kwa kununua mazao kwa bei ndogo na kusababisha wakulima kuendelea kuwa maskini.Chambanenge alisema kama Chama cha Mapinduzi kitamteua kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo na wananchi kumchagua kipaumbele chake cha kwanza itakuwa ni kuinua hali ya maisha ya kipato cha wananchi kwa kuboresha upatikanaji wa soko la mazao na kuifanya ardhi itumike kama rasmali ya kutoamitaji kwa wananchi.Awali Katibu wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mariamu Mwambanga, akizungumza na Nipashe kwa simu jana aliwataja wanachama wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kwela kuwa ni pamoja na Diwani wa kata ya Milepa, Ignas Malocha.Wengine ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya ya Kasuru mkoani Kigoma, Benedict Chapewa na Meja Jenerali Januari Kisanko.Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Sumbawanga vijiji walioongea na gazeti hili walisema DkMzindakaya ambaye amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30 amesoma alama za nyakati ndiyo maana ameamua kutangaza hadharani kuwa hana tena mpango wa kugombea nafasi hiyo ya ubunge.Walisema kwa vyeo ambavyo amewahi kushika katika nchi hii, inatosha kusema Dk. Mzindakaya anastaafu siasa akiwa na heshima nyingi za utumishi kwa wananchi wake na kwa Watanzania wote.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...