JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZA MKONONI
1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa nambazote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1 2009 hadiDesemba 31, 2009; na baadaye muda huo kuongezwa hadi tarehe30 Juni 2010 ikitamkwa wazi kuwa muda huo wa ujasilihautaongezwa tena. Sababu za kuanzisha utaratibu wa kusajilinamba za simu zimeelezwa mara kadhaa zikiwemo:(i) Kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma zamawasiliano(ii) Kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiapohuduma mbalimbali kama M – Pesa, Z-pesa, ZAP na hudumanyingine za malipo ya Ankara kama za Umeme, Maji,Televisheni n.k.(iii) Kuimarisha usalama wa nchi.(iv) Kuyawezesha makampuni ya simu kuwafahamu wateja waovizuri zaidi ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa hudumakwao.2. Wakati tunakaribia tarehe 30 Juni 2010, utaratibu umepangwakupitia Makampuni ya simu kuwa kuanzia tarehe 1 Juni 2010kuhakikisha laini yoyote itakayonunuliwa itatumika kwa kupiga aukupokea simu na kutuma au kupokea ujumbe ikiwa imesajiliwatu na si vinginevyo.23. Baada ya saa sita usiku tarehe 30 Juni yaani saa 00.00 kuanziatarehe 1 Julai, 2010 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwaitafungiwa kupiga ,kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi(SMS) kwa siku 90 hadi tarehe 30 Septemba 2010. Katika kipindihiki cha siku 90 endapo mtumiaji ataisajili namba yakeitafunguliwa. Kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapotarehe 30 Septemba zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandaokabisa.4. Mamlaka ya Mawasiliano imekubaliana na Makampuni ya simukufanya uhakiki wa usajili wa laini za simu za wateja kwa kutumianamba 106 kupitia simu za mkononi. Kwa wateja wa mitandaoiliyoko katika mifumo ya GSM, kama Zain, Vodacom, MIC (Tigo) naZantel, wateja wanatakiwa kuingiza *106# na kwa wateja wamitandao inayotumia mfumo wa CDMA kama BOL, TTCL mobile naSASATEL wateja watatakiwa kupiga namba 106 na watapokeataarifa za usajili.5. Hivi karibuni mswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki naposta ulipitishwa na Bunge kuwa sheria. Sheria hiyo inafanya usajiliwa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu washeria hio kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai. Adhabuni pamoja na faini au kifungo au vyote pamoja.6. Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuyashukuru makampuni ya simuna watumiaji kwa ushirikiano ambao wameonesha mpaka sasa kwaajili ya kufanikisha zoezi hili.Tunawasihi wote waendelee kusajililaini mpya kabla ya matumizi baada ya tarehe 30 juni 2010 nakuendelea kuhakiki laini zote zilizosajiliwa ili kukamilisha usajilikama ilivyokusudiwa.
Imetolewa naMkurugenzi MkuuMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Comments