Skip to main content

Tamasha la Nchi za Jahazi Laja

HAYA ni Mandhari ya mji wa Zanzibar.




ZIFF NI NINI

Tamasha la Nchi Za Jahazi ( ZIFF ) ambalo linatimiza miaka 13 mwaka huu ni moja ya matamasha makubwa Afrika Mashariki na linatambulika duniani kote kwa kuinua na kuendeleza filamu, muziki na sanaa za kiafrika katika majukwaa ya kimataifa..


LINI NA WAPI LINAFANYIKA

Julai 10-18, 2010

Kwa mwaka huu tamasha litaanza tarehe10 mpaka tarehe 18 ya mwezi wa saba(7), Kwa miaka mingi ZIFF imekuwa ikitumia Mji Mkongwe, hususani Ngome Kongwe kama jukwaa la matukio yote makubwa yanayotokea kwenye tamasha. Pia tamasha hufanyika katika mji wa Pemba na Tanzania Bara (Dar es Salaam na Bagamoyo).


ZAIDI KUHUSU ZIFF

Tamasha la Nchi za Jahazi ni moja kati ya matamasha makubwa ya utamaduni kwa ukanda huu wa Afrika mashariki. Kwa miaka 13 sasa ZIFF kimekuwa chombo cha jumuia ya kizanzibari yenye malengo ya kuendeleza filamu za kiafrika na pia kusherehekea utajiri wa tamaduni tofauti kutoka ndani na nje ya Afrika.


FILAMU


Kila mwaka ZIFF huleta pamoja maelfu ya watu toka hapa nyumbani, nje ya nchi, watengenezaji filamu toka Afrika na nje ya Afrika na wadau mbalimbali wa filamu kusheherekea tamasha hili la aina yake.

Kwa miaka mingi sasa ZIFF imeweza kujijengea jina kutokana na maonyesho makubwa yenye kuvuta hisia za wengi na kufanikiwa kuendeleza na kukuza wigo wa sinema katika Afrika na ughaibuni pia.


Tunalitangaza tamasha kwa kupitia watu maarufu na wenye majina (Mfano tumeshakuwa na wasanii mbalimbali kutoka Hollywood ambao hualikwa maalum kama wageni rasmi) lakini tunajivunia uwezo wetu wa kujitolea katika kuendeleza na kutangaza vipaji chipukizi katika sanaa na filamu za humu nchini.


UTAMADUNI



Ingawa kwa asili tamasha ni la filamu, ZIFF tunaamini katika nguvu ya sanaa, Hivyo tumeandaa ratiba itakayosheheni pia wasanii wa muziki waliochaguliwa kwa umakini mkubwa kutumbuiza ambapo muziki utakua ukipigwa “live”. Pia kutakuwa na maonesho ya sanaa, mwaka huu kutakuwa na maonesho ya Vitenge vya Wax toka Uholanzi, Ghana, Congo na Tanzania tukijivunia sanaa ambayo sasa ni biashara kubwa duniani kote.



JAMII

Maendeleo na ushiriki wa jamii umekuwa changamoto muhimu kwa ZIFF. Tumeweza kuwashirikisha na kuwaleta wanafunzi na vijana hasa kutoka shule za msingi na sekondari, na kwa hivyo kuwawezesha kupata nafasi ya kuangalia filamu za Kiafrika na za Kimataifa.


Kwa muda mrefu sasa Jukwaa la Wanawake ni jukwaa ambalo hujumuisha warsha na maonesho ya filamu ambayo hulenga kuendeleza majadiliano kuhusiana na shughuli za kijamii na haki za kisheria kwa wanawake. Vilevile jukwaa la wanawake huwapa fursa wanawake kujadili na kupanga mustakabali wao kama wanawake na pia kutambua uwezo na nafasi ya mwanamke katika kuendeleza jamii zao na zinazowazunguka.


Katika kutambua uwepo na kuthamini vipaji vya watoto ZIFF, kwa kushirikiana na Taasisi ya Filamu ya Denrmark, huwaletea watoto programu inayolenga kuendeleza na kuhamasisha uelewa na utengenezaji filamu kwa watoto.


SOKO

ZIFF ni tamasha muhimu kwa wadau wa filamu duniani kwa kuwa mwenyeji wa mabaraza ya kuunganisha, kusambaza, kuendeleza na kutangaza filamu, hasa za Kiafrika, ZIFF inaendeleza usambazaji filamu kwa watengeneza filamu kutoka nchi zilizoendelea na nchi za Afrika kwa kuimarisha soko la filamu.



MAFANIKIO YA MWAKA ULIOPITA 2009

Filamu ya Go With Peace Jamil (Afghanistan/Denmark) ambayo ilishinda tuzo ya SIGNIS na FIPRESCI mwaka jana iliweza kushinda pia katika tamasha la filamu la Goteborg baadae mwaka huo huo.


Bilal ( ya Sourav Farangi) nayo ilishinda tuzo katika tamasha la IFF Las Vegas pamoja na Aljzeera Golden Award (Aljazeera IFF)



Kaa tayari kwa filamu mpya zitakazozinduliwa mwaka huu ambazo HAUTAKIWI KUZIKOSA


Tunayofuraha kuwatangazia filamu mpya zitakazotambulishwa rasmi mwaka huu.


MOTHERLAND


Uzinduzi filamu mpya ya Motherland (ENAT HAGER) iliyoongozwa na mtayarishaji mahiri Owen Ailk Shahadah ambaye ni Mshindi wa tuzo ya PAN- AFRICAN film festival 2010, Makala bora.


MOTHERLAND ni filamu yenye mvuto inayogusa historia utamaduni na siasa ikisimulia hadithi mpya ya bara la Afrika ikiwa na wahusika kama vile Marais Meles Zenawi na Jacob Zuma na pia Mkufunzi maarufu Ali Mazuri na msanii Harry Belafonte.



TWIGA STARS: TIMU YA MPIRA WA MIGU YA WANAWAKE TANZANIA.


Kwa mapenzi na ushabiki mkubwa wa mpira wa miguu ambao unaonekana kukua kwa mwaka huu, ZIFF tunayo furaha kuwatangazia uzinduzi a filamu mpya ya TWIGA STARS, timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ni filamu iliyoandaliwa na Nisha Ligon.

Filamu hii inayoonesha maisha ya Twiga Stars, timu ya mpira wa miguu ya wanawake Tanzania kwa mwaka mzima, inaonesha uchaguaji, kambi za mazoezi na ushiriki katika mashindano nje ya nchi pia matatizo yote wanayokutana nayo wasichana ambao wana ari, vipaji na shauku kubwa la kujaribu kuwa wachezaji mahiri wa mpira wa miguu katika moja ya nchi maskini duniani.



FILAMU NYINGI ZITAKAZOONESHWA KWA MARA YA KWANZA NI..


MY POLICY FEATURE FICT PHAD MUTUMBA 2010 143MIN UGANDA/CANADA


LAMU'S MAULIDI DOCO CHABAI FEHD 2010 TUNISIA


INSIDE LIFE DOCO JULIA LANDAU 2010 48MIN SOUTH AFRICA


NIPE JIBU FEATURE FICT NADINE LOUISE FESER 2010 117MIN

TANZANIA/CANADA


WHERE IS MY DOG? MOCUMENTARY YOHANNES FELEKE AND MIGUEL LLANSO 2010

28MIN ETHIOPIA



TAARIFA ZAIDI

Kwa taarifa zaidi kuhusu ZIFF na tamasha la mwaka huu, tafadhali tembelea tovuti yetu www.ziff.or.tz/press au Kwa mawasiliano zaidi tafadhali tuma barua pepe kwenda press@ziff.or.tz


Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...