WANAHISA wa Benki ya NMB watapata gawio la jumla ya Shilingi 15.7 bilioni kwa mwaka 2009,
ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.7 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Misheck Ngatunga, amesema mgawo wa kila hisa kwa
mwaka utakuwa Shilingi 31.40, ikilinganishwa na Shilingi 30 kwa mwaka 2008.
Alikuwa anawasilisha ripoti ya mwaka 2009 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa NMB uliofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ngatunga alisema mwaka 2009 ulikuwa wa changamoto nyingi kutokana na kuongezeza kwa
ushindani katika sekta za benki pamoja na mtikisiko wa uchumi duniani, ambao ulikuwa na
madhara makubwa katika uchumi wa Tanzania kama kwingineko duniani.
Aliisifu serikali kwa kuandaa mkakati wa kukabiliana na mtikisiko wa uchumi kwa kuendeleza
mfuko wa kuokoa na kusaidia sekta na taasisi zilizoathirika na mtikisiko huo.
“Sekta ya fedha ya Tanzania kwa ujumla haikuathirika na mtikisiko huo, na iliendelea kuwa na
mtaji wa kutosha na yenye faida. Ingawa athari hizo zilikuwa tofauti kwa kila benki.”Hata
hivyo, alisema hali ya uchumi na kushuka kwa viwango vya riba vilichangia kushuka kidogo kwa
mapato na faida mwaka 2009, ambapo benki hiyo ilipata faida ya Shilingi 68.04 bilioni (kabla
ya kodi), ikilinganishwa na Shilingi 70.94 bilioni mwaka uliotangulia.
Upungufu huo wa faida ni kwa asilimia nne.Wakati huo huo, NMB imedhamiria kuboresha huduma
zake na kupunguza msongamo wa wateja katika matawi yake nchini na kuwafikia Watanzania wengi
zaidi wanaoshi vijijini.
Katika taarifa yake ya mwaka 2009, benki hiyo yenye mtandao mkubwa nchini imesisitiza kuwa
itazingatia zaidi kupunguza muda wa wateja kusubiri katika matawi na ATM, pamoja na
kuboresha mikopo.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi alisema pamoja na mafanikio mengi yaliyopatikana katika
kipindi kipindi cha mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa matawi na mtandao wa
ATM kutoka 167 mwaka 2008 hadi 281 mwishoni mwa mwaka 2009, bado wanakabiliwa na changa moto
nyingi, ikiwemo tatizo la msongamano wa wateja.
“Nina uhakika kwamba uongozi na wafanyakazi wa NMB watafanikiwa kukabiliana na changamoto
hizo,” alisema Ngatunga.Alisema NMB inakusudia kupanua zaidi mtandao wa matawi nchini ili
kuweza kujikita zaidi katika msukumo wa ‘Kilimo Kwanza’, mpango wa kuboresha uzalishaji wa
kilimo na sekta ya mabadiliko kwa nia ya mapinduzi ya kilimo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa NMB, Bern Christiaanse, alisema mtandao wa
matawi ya NMB uliongezeka kufikia 133 mwaka 2009, huku matawi mapya nane yakifunguliwa mwaka
huo.
Alisema ongezeko hilo ni matokeo ya mkakati wa benki hiyo wa kutoa huduma za kifedha kwa
watanzania wengi iwezekanavyo.Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2009, jumla ya raslimali za
benki hiyo zilikua kwa asilimia 20.6 kutoka Shilingi 1,384.3 bilioni hadi 1,669.3 bilioni,
wakati ambapo mtaji wa benki ulikua kwa asilimia 20.4 kutoka Shilingi 159,689 milioni hadi
Shilingi 192,239 milioni.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa NMB ni ya pili tangu benki hiyo
iwe kampuni ya umma baada ya kuorodheshwa kwenye soka la hisa la Dar es Salaam.

Comments