Skip to main content

Kesho Club Maisha Kufunguliwa Upya


Club Maisha inatarajiwa kufunguliwa upya Juni 24 mwaka

huu, baada ya kufanyiwa ujenzi mkubwa

kutokana na kuungua moto mwaka jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya

Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo,

Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu

hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga

nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika

kwa wateja wake.

“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa

kutoa burudani za usiku Dar es Salaam

iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na

inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani

za usiku.

“Baada ya miezi kadhaa wateja wetu kukosa

burudani, klabu yao sasa inarudi ikiwa ni ya

kisasa zaidi yenye televisheni 32 zitakazokuwa

zikionesha fainali za Kombe la Dunia na video

za muziki, sehemu mbili za kuchezea, vyumba

viwili maalumu vya VIP, hii yote ni katika

kuuweka kuwa ya kisasa,” alisema Majey.

Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni

pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya

juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa

inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na

michezo mingine kwa nje.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku

itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na

kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki

(ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani

ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa

sasa duniani.

“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka

Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme

Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali

ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya

dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama

mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.

“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club

Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za

usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa

lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda

burudani za usiku,” alisema.

Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo
ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000

kwa VIP. Tayari Jiji la Dar Salaam litaanza tena pilika pilika mpya kuanzia kesho kwani pande hizo zilikuwa zikitikisika vema kwa burudani ya disko hilo kabla ya ukumbi huo kuwaka moto.

Comments

Anonymous said…
I love club Maisha but i hate the way the djs fast foward songs... Why dont they play them the same way we hear and watch them from the redios and televisions???