Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika moja ya mikutano na wananchi wa jimbo lake hilo.
Akipokea zawadi ya kuku.
Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akikabidhi mashine ya kuvutia maji kwa wananchi wa moja ya kijiji katika Jimbo lake la Mvomero.
Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ameendelea na ziara ya kikazi jimboni kwake huku Makundi mbalimbali yaliendelea kumuunga Mkono na kumshawishi achukue fomu ya Ubunge kwa kipindi kijacho.
Katika ziara yake ya kichama amekagua kazi zinazotanywa na kikundi cha wakina mama wafinyanga vyungu, wakinamama wajasiriamali wauza kokoto na walima bustani.
Aidha
amezindua Shina la ushindi ambalo wakinamama wafinyanga vyungu ndiyo
wanachama wa Shina hilo, Katika kuunga Mkono vikundi hivyo mbunge
amewachangia pump ya kumwagilia na Fedha vyote kwa pamoja vinafikia sh 2,800,000.
Wakitoa
ujumbe kupitia nyimbo walimtaka mbunge wao muda ukifika achukue fomu
kwani wameridhishwa na kazi nzuri alizozifanya kijijini hapo ikiwepo
huduma za jamii.
Akihutubia
katika mkutano huo aliwapongeza kwa kujiunga katika vikundi na
mafanikio yanaonekana. Amewapongeza kwa bidha nzuri za majiko, vyungu na
upatikanaji wa kokoto kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Amewahakikishia ushirikiano wa dhati na atachukua fomu kutetea nafasi yake mara muda utakapofika.(Muro)
Comments