Siku ya Jumatatu, rapa, 37, ambaye albamu yake ya kwanza iliitwa The
College Dropout- alipokea shahada ya udaktari wa heshima kutoka kwenye
Taasisi ya Sanaa ya Chicago, kwenye mahafali yake.
Kanye alishindwa kuficha furaha zake wakati alipofika mbele chuoni
hapo – kinachofahamika kama moja ya chuo mashuhuri cha sanaa nchini –
ghafla akaondoa tabasamu hilo wakati alipokuwa nyuma ya jukwaa.
Ulikuwa wakati mzuri kwa Kanye, ambaye marehemu mama yake Dr. Donda
West alikuwa Profesa wa Kiingereza kwenye Chuo Kikuu cha Clark Atlanta,
baada akawa Mwenyekiti wa Idara ya Kiingereza kwenye Chuo Kikuu cha
Chicago.
Kwa sasa anajulikana kama Dr. West, Kanye alianza hotuba yake kwa
kusema: “Mimi ni msanii wa watu, hivyo lugha yangu ni maoni ya umma, na
ulimwengu ndio jukwaa langu.”
Comments