Papa Francis alikutana na rais wa Palestina Mahmud Abbas siku ya
Jumamosi, na kumuita “Malaika wa Amani” ikiwa ni siku kadhaa tangu
Vatican ijiandae kusaini makubaliano na Palestina na hivyo kuikasirisha
Israel.
Abbas alikutana na kiongozi huyo wa kidini kwa takribani dakika 20
faragha, makutano yanakuja baada ya Papa kujiandaa kuwatangaza makuhani
wawili wa Palestina na kuwa Waarabu wa kwanza Palestina kupewa
utakatifu.
Siku ya Jumatano Mtakatifu huyo alitangaza kwamba anajiandaa kusaini
mkataba wake na Palestina, miaka miwili baada ya kuitambua nchi hiyo
kama taifa.
Comments