Fellaini alieleza namna Mholanzi huyo, ambaye aliwasili akiwa na heshima kama kiongozi mwenye msimamo, ameagiza kuwepo na faini endapo wachezaji watakiuka maagizo, ikiwemo kulinda muda.
Akizungumza kuelekea mechi ya United dhidi ya Crystal Palace, Fellaini alisema: āAlifoka siku fulani wakati kikundi cha watu 10 kati yetu kilipochelewa dakika moja kula chakula cha mchana baada ya mazoezi.
āUnafikiri dakika moja si chochote na haikuwa kwa mazoezi, ila kwa ajili ya chakula. Kwake yeye ni jambo muhimu.
āAlitupiga faini. Hivyo ndivyo inavyotokea kwa wachelewaji hata kwa kadi nyekundu. Unatozwa faini, pia hata ukicheza rafu mbaya.ā
Comments