Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (katikati)
Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (kulia).
BENKI ya EximTanzania imezindua kampeni inayolenga kuwahamasisha wateja wake juu ya matumizi ya kadi zake mpya za 'Faida Chip and PIN Debit card' ambazo zimeundwa kwa kuzingatia vigezo vya kiusalama zaidi.
Kwa mujibu wa Meneja Bidhaa wa benki hiyo Bw. Aloyce Maro hatua hiyo ni sehemu ya jitiahada za benki hiyo kuhakikisha kwamba huduma zake zinatolewa kwa uhakika na usalama zaidi kwa faida ya wateja wake.
"Lengo
kubwa la kampeni hii ni kuwahamasisha wateja wetu juu ya matumizi ya
kadi zetu mpya za 'Faida Chip and PIN Debit card' ambazo zinatumia
'chip' badala ya 'magnetic strip' lengo likiwa kuongeza usalama wa
akaunti za wateja wetu'' alisema Bw. Maro wakati wa uzinduzi wa kampeni
hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Matumizi
ya kadi hizo yanaelezwa kuongeza usalama na amani miongoni mwa
watuamiaji wake kwa kuwa zina uwezo wakipekee katika kuhifadhi na
kutambua taarifa za mtumiaji na hivyo kuondoa hofu ya wizi wa namna
yoyote ile, kwa mujibu wa Bw. Maro.
"Kadi hii
inauwezo mkubwa wa kuhifadhi taarifa pamoja kumtambua mmiliki
wake.Uwezo huu ndio siri ya mafanikio yake kwa kuwa inauwezo wa kuwazuia
kabisa watu wenye nia ovu na akaunti ya mteja hususani kwa kufanya
jaribio la namna yoyote la wizi,'' alisema Bw. Maro.
Akiizungumzia
zaidi kadi hiyo Bw. Maro alisema inauwezo wa kumuwezesha mtumiaji wake
kuweza kuifikia akaunti yake na kufanya miamala kutoka kwenye mashine za
kutolea fedha zenye uthibitisho wa 'MasterCard' pamoja na zile za POS
ulimwenguni kote bila usumbufu wowote.
Aidha Bw.
Maro aliwahamasisha wateja wa benki hiyo ambao bado hawajachukua kadi
zao wajitokeze kuzichukua kwenye matawi ya benki hiyo ili waanze kufaidi
matumizi yake.(Muro)
Comments