Wakazi wa mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelalamikia mauaji ya watu wengi yaliyotokea hivi karibuni katika mji huo.
Wakazi wa mji huo jana walisitisha kazi zao zote kama ishara ya kulalamikia mauaji hayo ya umati.
Wakazi wa mji wa Beni wanavilaumu vikosi vya serikali ya nchi hiyo kushindwa kuwalinda raia.
Gilbert Kambale
mmoja wa viongozi wa asasi za kiraia amesema kuwa, wakazi wa mji huo
wataendelea kusimamisha shughuli zao za kawaida kwa muda usiojulikana na
kwamba, wanaitaka serikali imfute kazi kamanda wa vikosi vya serikali
vya Operesheni ya Sukola-1 kutokana na kushindwa kulinda roho za watu wa
mji huo.
Comments