Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair ametangaza kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Umoja wa Kimataifa kwenye kamati inaoshughulikia usuluhishi wa migogoro ya Mashariki ya Kati Quartet. Migogoro hiyo inahusisha nchi ya Israel na Palestina nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka nane tangu mwaka 2007 akiwakilisha pande nne yaani Marekani, Russia, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.
Blair
alimwandikia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusu
kujiuzulu kwake na kuahidi kusaidia Jumuiya ya Kimataifa katika kazi
zinazohusu Israel na Palestina katika siku zijazo.
Vyanzo
vya habari vilivyokaribu na Blair vinasema, ataendelea kuwepo
akijihusisha na baadhi ya shughuli na eneo hilo. Watoa habari hao
wanasema kuwa waziri mkuu huyo wa zamani anaamini kuwa mtazamo mpya
unahitajika.
Lakini
wakosoaji wanasema Blair alipambana katika jukumu ambalo lilikuwa na
mipaka katika maendeleo ya kiuchumi na ameshindwa kuleta matokeo chanya.
Ofisa mmoja wa Palestina amemlaumu Blair kwa kufanya kazi kwa upendeleo ili kuwaridhisha Waisrael na Marekani.
Kamati hiyo ya Umoja wa Kimataifa inaoshughulikia migogoro ya Mashariki ya Kati unaundwa na UN, EU nchi ya Marekani na Urusi.
CHANZO:BBC
Comments