Wanamgambo 60 wa Boko Haramu wameuawa katika mapigano na wanajeshi wa Cameroon karibu na mpaka wa Nigeria.
Afisa wa jeshi la Cameroon Aboubakar Issa, ametoa
taarifa hiyo kwenye shirika la Anadolu akisema” Karibia
wanamgambo 100 walivuka mpaka kwa kutumia pikipiki Jumamosi usiku,” na
kushambulia mji wa Zelevet uliopo kusini mwa Cameroon.
Aliongeza kusema kuwa,walishambulia kambi ndogo ya kijeshi katika mji wa Kalashnikovs, na kuwaua askari 2 huku wanamgambo 60 wakiuawa.
Boko Haram,
wameongeza mashambulizi nchini Cameroon katika miezi ya hivi karibuni na
kusababisha mamlaka ya ulinzi ya Cameroon kuongeza vikosi vya ulinzi
mpakani mwa Nigeria kwa msaada wa vikosi vya Chad mwezi Januari.
Nchi ya Cameroon
imejiunga pamoja na Nigeria na Majirani zake ikiwemo Niger na Chad
katika kupambana na mashambulizi dhidi ya Boko Haram.
Comments