Kocha wa Yanga, Hans Van der Pluijm ameonekana kuvutiwa na wachezaji wawili wa Simba Ramadhani Singano na Said Ndemla.
Kocha huyo amesema kuwa endapo atafanikiwa kukamilisha dili la
kuwasajili nyota hao basi atakuwa amemaliza tatizo la mshambuliaji
anayetumia mguu wa kushoto.
Hans ameongeza bidii ya kuhitaji huduma ya mchezaji Singano baada ya
kupata taarifa kuwa mchezaji huyo amemaliza mkataba wake na wekundu wa
msimbazi ambapo amehudumu kwa misimu mitatu.
Inasemekana kuwa uongozi wa Yanga tayari umeshakutana na Messi na kufanya naye mazungumzo, lakini huenda kukawa na upinzani mkali baada ya Azam nao kuonyesha nia ya kutaka huduma ya mshambuliaji huyo msimu ujao.

Comments