Kundi la Al-Shabaab limetangaza kumpoteza kamanda wake Sheikh Hassan Turki aliyekuwa anasakwa na Marekani.
Kwa taarifa iliyotolewa na msemaji wa kundi hilo Ali Mohamud Rage alisema kamanda Sheikh Hassan Turki mwenye umri wa miaka 73 aliaga dunia nyumbani kwake katika kijiji cha Hargeysa Yarey baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Sheikh Hassan Turki alikuwa kiongozi wa muungano wa Mahakama za
Kiislamu nchini Somalia, alijumuishwa kwenye orodha ya watuhumiwa
wanaotafutwa na Marekani kwa madai kuwa alikuwa analifadhili kundi hilo.
Comments