Tim Sherwood amekubali kuwa hana nguvu ya kumzuia Christian Benteke
kuondoka Aston Villa msimu huu baada ya mshambuliaji huyo Mbelgiji
kuzungumzia mkataba wake.
Liverpool wako tayari kumnasa Benteke, ambaye amefunga magoli 12
katika mechi 14 tangu Sherwood atue, Sportsmail inaelewa kuwa pauni
milioni 32.5 zitamfanya aondoke.
Fainali ya Kombe la FA Jumamosi dhidi ya Arsenal uwanja wa Wembley utathibitisha mwisho wa Benteke kuvaa fulana ya Vila.
Comments