Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amevishukuru vikosi vya jeshi
vinavyo mtii kwa kuzuia jaribio la kumpindua huku akitoa onyo la
kumalizwa kwa maandamano yanayoendelea nchini humo.
Bwana Nkurunziza pia ameshtumu maandamano hayo pamoja wale walioshiriki jaribio la mapinduzi .
Bwana Nkurunziza pia ameshtumu maandamano hayo pamoja wale walioshiriki jaribio la mapinduzi .
Rais Nkurunziza pia amewaomba wananchi kuchangia mfuko wa uchaguzi
kutokana na kutokuwepo fedha za kutosha kuendesha uchaguzi huo.
Katika hatua nyingine, marais wanne wa zamani wa Burundi, wamepinga
hatua ya Rais Pierre Nkurunziza, kuwania awamu ya tatu huku wakikiri
kuwa ni kinyume cha katiba.
Maraisi hao wameonya hatua hiyo kwamba inaweza kuvuruga amani
iliyopatikana baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka
2006.
Marais hao wanne waliotia saini barua yao ya kumpinga Nkurunziza, ni
Jean-Baptiste Bagaza, Sylvestre Ntibantunganya, Pierre Buyoya, na
Dominitien Ndayizeye.
Marais hao walitawala Burundi, katika kipindi cha miaka ya 1976 na
2005, wakati Nkurunziza, alipoingia rasmi madarakani kwa kura ya Bunge.
Bwana Nkurunziza, alirejea jijini Bujumbura leo baada ya jaribio la kumwondoa madarakani kushindikana.
Comments