Kiungo mahiri wa Simba, Jonas Mkude amesema kuwa ujio wa kiungo Peter
Mwalyanzi katika kikosi chao ni bab’kubwa na kuwatambia wapinzani wao akisema
mbona mtatukoma!
Mkude alisema ujio wa Mwalyanzi utatengeneza Simba mpya ambayo haitakuwa rahisi kuzuilika sambamba na kuifanya iwe inacheza soka la kuvutia litakalokuwa likitoa matokeo mazuri kwao.
Mwalyanzi amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba akitokea Mbeya City na moja kwa moja ameingia kwenye idara ya kiungo ya Simba iliyokuwa inatawaliwa na Jonas Mkude.
Mkude ameliambia mwanaspoti akisema: “Huyo jamaa (Peter Mwalyanzi) ni mmoja wa viungo mafundi, ninawakubali sana, si kwa kukimbia bali upigaji wa pasi na umiliki wa mpira.
“Nimeshacheza dhidi yake akiwa Mbeya City kama mara tatu, acha kabisa, mziki wake si mchezo. Kwa kweli ninawapongeza viongozi kwa kutuletea bonge la mchezeshaji. “Sasa Simba itakuwa ni mwendo wa kupiga pasi nyingi, kupiga bao na kutwaa ubingwa. Naamini leo hii anakuja kuongeza nguvu kubwa kwenye kikosi chetu, sisi wachezaji tunampokea kwa mikono miwili na tutampa ushirikiano wa kutosha. Mwalyanzi karibu Simba,” alisema Mkude nahodha msaidizi.
Mwalyanzi alitua Simba juzi na kusaini mkataba wa miaka miwili, akiwa ndiye mchezaji wa kwanza kusainishwa Msimbazi nje ya wachezaji walioongezewa mkataba wa klabu hiyo iliyoshika nafasi ya tatu baada ya msimu uliopita kukamata nafasi ya nne.

Comments