Skip to main content

SOMA RATIBA YA DK SLAA KUANZIA KESHO ANAVYOIZUNGUKA TANZANIA


Kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa Katibu Mkuu, Dk. Willibroad Slaa atafanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi, ambapo atakuwa na shughuli kadhaa, ikiwemo kukagua mwenendo wa uandikishaji wa wapiga kura unaofanyika kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR).


Katika ziara hiyo ya siku 6 kuanzia Jumamosi ya Mei 30, 2015, Katibu Mkuu Dk. Slaa mbali ya kujionea zoezi hilo la BVR katika vituo vya uandikishaji, atafanya mikutano ya hadhara kwenye maeneo yote atakayozuru ambapo atazungumza na wananchi juu ya masuala yanayowahusu katika maeneo yao pamoja na mengine ya kitaifa.

Kupitia shughuli hizo atakazofanya, Katibu Mkuu ataendelea kuwahamasisha Watanzania wenye sifa za kupiga kura, kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) linalofanyika maeneo mbalimbali nchini kwa kutumia mfumo wa BVR.

Aidha, Katibu Mkuu Dk. Slaa atatumia fursa hiyo kukagua shughuli mbalimbali za chama zinazofanywa na viongozi na watendaji wa CHADEMA katika kanda za chama; Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo inajumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma Rukwa pia Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi.

Katibu Mkuu pia atapata fursa ya kukutana na viongozi na watendaji wa chama wa ngazi za chini katika kanda hizo na kusikia kutoka kwao namna wanavyoendelea kutekeleza programu na mikakati waliyojipangia katika maeneo yao au kuelekezwa na vikao vya chama, ikiwa ni sehemu ya kuzidi kukiandaa chama na UKAWA yaani vyama vinne (NLD, NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA), kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ratiba ya ziara ya Katibu Mkuu Dk. Slaa itakuwa kama ifuatavyo;
1.      Jumamosi Mei 30, 2015 - Mbozi (Vwawa) atafanya mkutano wa hadhara Uwanja wa Ichenjezya.
2.      Jumapili Mei 31, 2015 – Tunduma- Mbeya, atafanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.
3.      Jumatatu Juni 1, 2015 – Sumbawanga- Rukwa, atafanya mkutano wa hadhara Uwanja wa Stendi ya Chanji, mjini Sumbawanga.
4.      Jumanne Juni 2, 2015 – Mpanda Mjini- Katavi, atafanya mkutano katika Uwanja wa Kashaulili.

Itakumbukwa kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa alifanya ziara ya siku 3 hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera ambako alishuhudia udhaifu na mapungufu makubwa katika uandikishaji wa BVR, ikiwemo wananchi kutishwa, kupigwa, kuzuiwa kujiandikisha na viongozi wa CCM wakiwa vituoni, mashine kutofanya kazi, siku za kuandikishwa kutojulikana na uandikishaji kufanyika ‘electronically na manually’ bila maelezo yoyote kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Imetolewa leo Ijumaa, Mei 29, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

CHADEMA

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. Sławomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...