Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kina dalili zote za
kujiengua kutoka kwenye umoja wa vyama vya siasa vinavyotokana na Umoja
wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), gazeti la TAIFA IMARA linachambua.
CHADEMA imeonesha dalili tatu za wazi za kujiengua kutoka kwenye
umoja huo kabla ya kufikia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatatu ya
Oktoba 25, mwaka huu baada ya kuanza kufanya maandalizi ya uchaguzi huo
kivyake na kutofautiana kimsimamo juu ya kujiunga kwa chama cha siasa
cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Zuberi Kabwe.
Dalili ya kwanza ya CHADEMA kujiengua kwenye UKAWA ambao ni umoja
shinikizi wa kikatiba ulioanzishwa Februari mwaka jana, kwa kuvihusisha
vyama vyingine vya CUF, NLD na NCCR-Mageuzi ni kushindwa kuheshimu
utaratibu mpya wa kuachiana na majimbo ya uchaguzi.
Hilo linatokana na ukweli kwamba, chama hicho imeanza mchakato wa
kuorodhesha wanachama wake wasomi wanaotaka kuwania ubunge na udiwani
kwenye maeneo mbalimbali bila kujali kwamba maeneo hayo kuna wabunge wa
vyama vingine kama vitasimamisha mgombea kwenye maeneo hayo au la.
Chanzo: Taifa Imara
Comments