Harry Kane ni mshambuliaji wa juu kwenye orodha ya wachezaji wanaowania na Manchester United kwenye majira haya ya joto.
Louis van Gaal ameshatambua idadi ya wachezaji atakaojiandaa nao
wakati United itakaporejea Ligi ya Mabingwa, akiwemo mshambuliaji,
mlinzi wa kulia, wa kati na kiungo wa kati wako kwenye rada yake.
Tayari anaye winga Memphis Depay lakini Kane, ambaye amekuwa mchezaji
wa kwanza kuifungia Tottenham Spurs magoli 30 kwenye msimu baada ya
Gary Lineker, ni mshambuliaji ambaye kocha wa United anamhitaji pamoja
na kwamba 21, alisaini mkataba wa miaka mitano na nusu Februari.
Manchester United wanatarajia kutoa zaidi ya pauni milioni 46 kwa
ajili ya Kane, ambaye ameshiriki kiasi kikubwa katika matangazo ya jezi
mpya za Spurs.
Comments