Hatimaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo hii
limekubali kuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame.
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA ambao ndio wamiliki wa mashindano haya watatoa mialiko kwa klabu zenye sifa ya kushiriki na wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya klabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo.

Michuano hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Julai 11 hadi Agosti 2, mwaka 2015.
Comments