Marekani yajiandaa kutuma wakufunzi wa kijeshi nchini Nigeria
kumsaidia vikosi vya kijeshi vya rais mpya Muhammadu Buhari kukuza ujuzi
wao wa kijasusi.
Hali mbaya kati ya washauri wa jeshi la Marekani na jeshi la Nigeria
dhidi ya ukiukwaji haiza binadamu na rushwa chini ya rais aliyeshindwa
Goodluck Jonathan uliathiri jitihada za kupambana vita ya miaka sita ya
Boko Haram
Maafisa wa Idara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema Buhari na Waziri
wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry watajadili mustakabali wa msaada
wa kiusalama na kupanua mshikamano wa kiuchumi katika mkutano baada ya
kuapishwa kwa rais huyo Ijumaa.
Maafisa wamezungumzia hali ya sintofamu kuhusu ziara ya Kerry mjini
Abuja, walisema mazungumzo na Buhari yameonyesha “ushirikiano wa karibu”
na Marekani.
“Tuna kila dalili kwamba tutakuwa na uwezo wa kuanza mwanzo mpya.
Tunaendelea kuwa na washauri pale…. Ninachokizunumza ni kuwa tutakuwa na
washauri wapya pale tutakapopapanua.”
Comments