(PICHANI ) aliyevalia flana ni Mh Mbunge wa Ilala Mssa Azzani Zungu katikati na wakwanza kulia ni Zahir Baba leo katika mazungmzo na watoto waishio katika mazingira magumu hapa ni
viwanja vya Posta Mpya Dar es Salaam.
UMOJA WA WATOTO TUNAOISHI KATIKA MAZINGRA MAGUMU (MITAANI)
Mh mgeni rasmi Mussa Azzani Zungu wageni waarikwa wote mliofika hapa hii leo wote tunawakaribisha lakini pia ni furaha kwetu kuwaona mmefika hapa , siku hii ya leo,
kwa kweli mnaitaji pongezi za pekee siku hii ya leo.
Mh mgeni rasmi katika umoja huu kuna watoto na vijana ambao wote tunaishi maisha ya kubahatisha kutokana na kukosa mahitaji muhimu kama vile chakula makazi na elimu kwa binadamu.
Tumeamua kuunda umoja ili tuweze kuomba msaada na tusaidiwe ilikuondokana na maisha haya mabaya.
Maelezo Yetu :
Mh mgeni rasmi sisi tumetoka sehemu mbalimbali ndani ya tanzania .
Sababu zilizotufanya kuondoka majumbani mwetu ni nyingi lakini moja ya sababu hizo ni ugomvi wa wazazi , umaskini , kufiwa na wazazi kutelekezwa na ndugu.
Mh mgeni rasmi watoto ukimbia majumbani baada ya kuona hali imekuwa mbaya hukimbilia mijini kwa kujua kwamba wanaweza kusaidiwa na jamii.Mh mgeni rasmi watoto wengi hawana elimu hata ya shule ya msingi na wengine wameshindwa kumaliza baada ya kutokewa na matatizo kama haya niliyosema.
Maranyingi wazazi wanapogombana baba au mama , mzazi mmoja wapo anakimbia familia baadaye mtoto anajikuta anaishi na baba wa kambo au mama wa kambo hii nayo uchangia sana watoto kupata mateso na shida kubwa katika maisha haya.
Vile vile mtoto anapofiwa na mzazi mmoja mfano baba katika familia maskini , mama ushindwa kulea familia.
Lakini vile vile mtoto anapofiwa na wazazi wote yaani baba na mama, mtoto ukaa na famila na mara nyingi familia umtelekeza mtoto na kuonekana hana maana tena
Hii ni moja ya sababu ya watoto kujikuta wanaishi maisha haya.
DHUMUNI LA MKUTANO HUU
Mh mgeni rasmi baada ya kuona tunaishi mitaani tu , bila mafaniki yoyote kwetu na Taifa letu na sisi tukiwa kama watanzania tumeona tujitokeze mbeleyenu ilimtusaidie tuweze kujiendeleza kimaisha .
Mh mgeni rasmi sisi bado ni nguvu kazi tunajua kuwa kwamba tunadeni kubwa kwetu na Taifa letu la Tanzania hivyo kuendelea kuishi mitaani ni kupoteza muelekeo wetu.
Mh mgeni rasmi kwa sasa tulikuwa tunaomba tupatiwe sehemu maalum kwa ajili ya makazi hata ya muda kwanza lakini pia , tupatiwe utaratibu wa kupata elemu hata ya shule ya msingi . Tumechoka kuendelea kulala nje na kuonekana kero katika jamii.
Lakini pia kumuomba mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndu Jakaya Mrisho Kikwete kutafuta njia mbadala wa kumaliza tatizo hili la watoto kama sisi endapo tutapata malezi bora tunaweza kusoma elimu ya msingi na hata chuo , pia tukiwezesghwa kupata elimu hata ya Ufundi Stadi .
Tunaweza kujiajili sisi wenyewe ila kwa sasa tunaomba kwenu mkiwa kama wazazi tupatiwe nyumba ya kulala hata ya muda hili tunapo zunguka tujuwe tunalala wapi .
CHANGA MOTO TUNAZO PATA
Mh mgeni rasmi kunachanga moto nyingi tunazo pata katika maisha haya lakini moja ya changamoto hizo ni ukosefu wa chakula , maranyingi watoto ula mabaki ya chakula cha mahotelini au makoko .
Watoto ulala nje bila shuka wala godolo na kupelekea kuugua mangonjwa mbali mbali kama vile maralia. Mh mgeni rasmi kunachangamoto nyingi sana kwani hata tunapokwenda kwenye vituo vya kulelea watoto hatupati nafasi za kukaa kutokana na kudai kuwa hawana nafasi pia inapotokea mtoto anaumwa atuna msaada wowote kituambacho upelekea watoto kufa ovyo bila msaada wowote.
MAFANIKIO
Mh mgeni rasmi mafanikio tuliyoyapata tangu kujumuika kwetu ni pamoja na kusikilizana sisi kwa sisi kuwaelimusha wenzetu kuachana na madawa ya kulevya kwa wale wanaotumia lakini pia , kuweza kukupata wewe mh mgeni rasmi na wageni wengine waalikwa hiinayoni mafanikio kwetu.
SHUKRANI
Mh mgeni rasmi kwanza kabisa napenda kumshukuru mwenyezi mungu kuweza kutukutanisha hapa leo hii tena kwani bila yeye yote ni bure lakini pia tunawashukuru wote mliofika hapa leo hii bila kutuzadharau .
Napenda kuku shukuru wewe Mh mgeni rasm pia napenda kukushukuru Ndugu Dr kafumu na Ndugu Zahir Baba kwa ushirikiano wenu mzuri mungu atawalipa endeleeni
na moyo huu wa upendo .
HITIMISHO
Mh mgeni rasmi pamoja na maelekezo yote haya ni vyema mkajua kuwa sisi mpaka sasa tupo katika wakati mgumu endapo kunatokea tatizo hata la mtoto kuumwa akuna sehemu, tunayojua kuwa tutaenda kusaidiwa.
Mh mgeni rasmi hata ofisi hatuna ya kusema tuwe tunakutana tumekuwa tukilala nje siku zote hivyo mvua zetu na jua letu mpaka lini nduguzanguni.?
Tumechoka kuonekana kero katika jamii ,tumechoka kuonekana kwenye mataa ya magari ambapo tunaenda kuomba misaada kwa ajili ya matumizi ya chakula tunataka kukaa sehemu moja ilitusome kwa faida yetu na taifa letu.
Tunaomba sana tusaidiwe hata nyumba moja kubwa tukapangishiwa hitakuwa vizuri sana, kwani watoto wadogo wa miaka tisa na kuendelea kulala nje kuna tuathili sana afya zetu lakini pia tunaomba msaada wa chakula walau mlommoja kwa siku katika kipindi hiki kigumu cha sasa.
Asanteni sana kuweza kunisikiliza kwa lisala yetu hii kama kuna mapungufu mtatusamehe lakini ni imani yetu tuta kuwa tumeeleweka mungu wabariki wote waliofika hapa siku hii ya leo.
KAULI MBIU MTOTO WA MWENZIO NI MTOTO WAKO MPENDE NA MTHAMINI .
Comments