Onesho kabambe la mavazi Mavazi la Lady in Red kutoka Fabak Fashions laja ,Asia Idarous kati akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi ndani ya hoteli ya Regency Park, kuhusiana na onesho hilo ambalo limepangwa kufanyika kesho jumamosi Februari 6 kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempiski Hotel,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 20,000/= kwa kila kichwa.Kulia ni Mmoja wa wabunifu mahiri hapa bongo Ally Rhemtullah,Muwakilishi wa kampuni ya Darling Julius Ngatunga na shoto ni Muwakilishi kutoka New Habari House Peter Mwendapole.
Asia amesema kuwa katika onesho hilo kutakuwepo na burudani kabambe kutoka bendi ya Machozi Bang ikiongowa na Lady Jay D pamoja na kikundi cha ngoma za asili Simba Traditional Dance,aidha pia wabunifu 16 mahiri wataonyesha ubunifu wao wa mavazi ambao ni Faruk Abdella,Manju Msita,Khadija Mwanamboka,Ally Rhemtullah,Mustafa Hasanali,Zamda George,Jamila Swai,Gymkana,Farha Sultan,Baraka,Fransisca,Bianca,Hiari,Joice,Salim Ali na Martin Kadinda.
Aidha Mwaandaji huyo ameongeza kuwa katika mchakato huo pia kutakuwepo na tuzo ta mbunifu bora wa mwaka 2010,tuzo ya Miss Beauty with purpose.
Kama vile haitoshi kutakuwepo na mnada kwa ajili ya kusaidia/changia watoto yatima wa Mitindo House pamoja.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Darling Hair,Redd's,Utrack Total Control,Valye Spring,BenchMark Production,Sofia Produtcions,Michuzi Blog,Kitangoma Magazine,Zizzou Fashions,Jiachie Blog,8020 Blog,Kitangoma Magazine,Clouds Fm na wengineo kibao.
Posted by kingkif at 3:54 PM 0 comments
Zanzibar International Film Festival (ZIFF) - 2010.
ZIFF 2010-HOPES IN HARMONY-CALL FOR ENTRIES
Zanzibar International Film Festival (ZIFF) - 2010.
Tamasha la 13 la Nchi za Majahazi linapenda kuwangazia wadau wote wa filamu nchini kuwa milango iko wazi kwa wao kuwasilisha filamu zao kwa uchaguzi wa kuoneshwa katika Tamasha la ZIFF.
Filamu zipokewazo ni Short, Feature, Documentaries na AnimationWadau tumeni Filamu zenu kabla ya 31 March, 2010.
Hii ni kwa filamu zilizotengenezwa kuanzia mwaka 2008 mpaka 2010
Fomu zinapatikana katika
www.ziff.or.tz
Tuma filamu yako sasa!
Kwa maelezo Zaidi wasiliana na Daniel Nyalusi
Events and Film Program Coordinator
Zanzibar International Film Festival
filmdept@ziff.or.tz
+255 655 940094
Comments