Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. William Lukuvi akizungumza jioni hii Ofisini kwake wakati alipokuwa akiwahamasisha wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 13 februari 2010 kwenye viwanja vya Leaders Club ambako tamasha kubwa la uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza malaria iliyopewa jina la "Zinduka" litafanyika ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo.
Mkuu wa mkoa huyo amewataka watu mbalimbali katika maeneo ya jiji la Dar es salaam kujitokeza ili kushirikiana kwa pamoja na mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.
Wasanii mbalimbali ambao wamechaguliwa kuwas mabalozi wa kampeni hiyo wataimba siku hiyo na kushirikisha wasanii wengine pia kwa pamoja ili kutoa ujumbe wenye kuhamasisha jamii kutumia vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa Maralia, na bbaada ya kumaliza Dar wasanii hao wataendelea na kampeni hiyo kwa nchi nzima katika kuhamasisha mapambano dhidi ya Maralia
Kampeni hiyo inaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikishirikiana na taasisi ya Malaria No More ya nchini Marekani ili kuhakikisha ugonjwa huo unapungua kwa kiasi kikubwa .
Comments