IBRAHIM kamwe alianza ngumi akiwa anasoma sekondari , baada ya kusoma shule ya msingi Upanga 1987 hadi mwaka 1986 ambapo alitia timu shule ya Sekondari Tambaza baada ya kufaulu mtiani ambapo alisomavidatu viwili na kuhamia Alaalamain na kumaliza mwaka 1992 alipomaliza kidatu cha nne.
Alianza kupigana ngumi za Ridhaa mwaka 1987 Anatogo , mpaka mwaka 1991 na mwaka uliofuata aliitimu Dar Techinique.
Mapambano aliyowahi kucheza ni ya uzito wa Kg 57 ambapo aliwahi kuichapa na Ally Baba , Said Chaku Papa Upanga .
Alisha pigana pia ngumi za kulipwa nchini Uingereza katika mapambano manne .
Jamaa kanieleza mengi sana kuhusu masuala ya ngumi jana nyumbani kwake Mwananyamala A jijini Dar es Salaam.
Alichonga kuwa katika mapambano yote alipokuwa akizichapa uko Ughaibuni alicheza katika uzito wa Kg 71 ambao ni uzito mwepesi (Light Mido).
Kwa sasa ni mudau anapromoti mapambano ya ngumi , nchini amebaatika kujenga nyumba anayoishi hapo Mwananyamala A akiwa na familia yenye watoto wawili mtoto wake wa kwanza anaitwa Abdul na wapili anaitwa Abass mwenye miezi minne tangu azaliwe watoto wakwe wote amezaa na mkewe Rahama Said .
Comments