Stori
ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa mkongwe wa Hip Hop Joseph Haule aka
Professor Jay ambaye wiki zilizopita alishinda kura za maoni kupitia chama cha
Demokrasia na Maendeleo katika Jimbo la mikumi Morogoro.
Profesa
Jay alisema maneno haya mara baada ya kupata ushindi huo
‘Namshukuru
Mungu kura za maoni zimeenda vizuri, niwapongezi tu watu wa CHADEMA kwa
kutimiza demokrasia na tuliweza kupga kura na nimeweza kuibuka mshindi baada ya
kupata kura 240 n Mpinzani wangu DR. Salvatory Makweta 18, Brendan Maro
15, Mkumbata 5 lakini niseme kwamba ule ushindi sio kuonesha Jay ameshinda au
anajua sana nawashukuru sana watia nia wote walikuwa wana nguvu na wote
walikuwa na uwezo’- Professor Jay
‘Baada
ya kushinda kura za maoni nimepita kuwashukuru wananchi kwa kunichagua wajua wa
kamati kuu zile za kata lakini pia nimewaomba watia nia wenzangu wahusike moja
kwa moja kwenye hizi kampeni na kwa moyo wamekubali na ndio wataendeza kampeni
zangu kwasababu naamini kupitia elimu zao kila kitu kitaenda sawa’ – Professor
Jay
‘Pamoja
nimechaguliwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mikumi kazi zangu za
Muziki nitaendelea kuufanya kwasababu muziki ndio maisha yangu na nitakufa
nikiendelea kufanya muziki ila nitakuwa sifanya kwa mashindano bali muziki
wangu utakuwa wa Level juu kwa hiyo nitakuwa nafanya mara chache kwa level ya
juu zaidi, mashabiki wangu watambue kuwa nipo kwaajili yao na sitawangusha’ –
Professor Jay
Comments