Msanii wa bongo fleva Nay wa Mitego amefunguka na kusema namba za
966 kwenye nyimbo zake, atakua akitumia namba hizo hata katika magari
yake.amesema huwa anatoa oda na kusubiri…Ni kitu ambacho ameamua iwe hivyo kwa gharama yoyote ile
Ney wa mitego amesema “Yan iko hivyo, gari
zangu zote nitakazonunua zile ndio namba zangu, hata baadhi ya vitu
vyangu vya usajili huwa nasajili kwa namba zile pia hata tin namba yangu
ni hivyo hivyo yan, niliomba hivyo na nimeisajili hivyo,so ni namba
ambazo zimeshakuwa official kwamba ndio namba zangu“.
Alipoulizwa kuwa huwa anafanya nini kama akiagiza gari na namba
zikiwa bado hazijafika! Ney alisema “huwa nasubiri kwa sababu huwa ni
order ambayo natoa na ninaihitaji zile namba huwa nasubiri hivyo”.
Comments