Matokeo ya kura za maoni kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi kwa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge yameendelea kuwa
mwiba mkali kwa waliokuwa wakitetea nafasi hizo.
Mbunge wa Kilombero Abdu Mteketa
Wilayani
kilombero aliyekua mbunge wa jimbo hilo Abdul Mteketa amelazimika
kuyakimbia matokeo baada ya kubaini ameangushwa katika kutetea nafasi
hiyo.
Hali hiyo imejitokeza wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi
ndani ya CCM, wa kuwatafuta wawakilishi wa ubunge na udiwani
watakaopeperusha bendera ya CCM, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka
huu,
Mbunge wa Kilombero Abdu Mteketa alilazimika kususia zoezi hilo baada
ya kubaini nafasi aliyokuwa akiwania kuitetea, kuchukuliwa na kijana
mdogo, Abubakar Asenga aliyetumia nafasi hiyo kuwaomba wana ccm kuvunja
makundi yaliyojitokeza wakati wa kura za maoni na kuwa wamoja ili
kufanikisha ushindi na maendeleo ya chama hicho na taifa kwa ujumla
Abubakar Asenga ameshinda kura hizo za maoni za kuwania ubunge
kilombero kwa kupata kura 9629,dhidi ya mpinzani wake wa karibu Abdalah
Lyana aliyepata kura 3999 huku mteketa aliyekuwa akiwania nafasi hiyo
akishika nafasi ya tatu kwa kuambulia kura 2646 na alipotafutwa kwa
simu yake ya mkononi iliita bila majibu,
Katibu wa CCM, wilaya ya kilombero Bakari Mfaume pamoja na kushukuru
zoezi hilo kumalizika salama,amesema ofisi yake ipo tayari kupokea
malalamiko ya wanaodhani wameonewa katika uchaguzi huo ili wafanyie
kazi.
Katika maeneo mengine ya uchaguzi ndani ya ccm mkoani Morogoro,baadhi
ya waliokuwa wabunge wamefañikiwa kutetea nafasi zao kwa kushinda kura
za maoni,akiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Haji Mponda aliyeshinda jimbo la ulanga magharibi,Waziri wa nchi ofisi
ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa umma,Celina Kombani akishinda ulanga
mashariki,Ahmed Shabiby akishinda jimbo la Gairo na Abdulaziz Abood
akishinda Morogoro mjini,huku jimbo wazi la kilosa ambalo awali
lilishikiliwa na Mustafa Mkulo ambaye hakugombea tena akishinda Mbaraka
Bawaziri.
Walioangushwa ni pamoja na naibu waziri wa maji na mbunge wa mvomero
amos makala na nafasi hiyo kuchukuliwa na aliyewahi kuwa mbunge wa
jimbo hilo suleiman Sadiq Murrad,aliyewà hi kuwa Naibu Waziri wa afya
Dkt. Lucy Nkya akianguka jimbo la Morogoro kusini Mashariki na nafasi
yake kuchukuliwa na Mgumba,
Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Morogoro Innocent Kalogores akiangushwa
jimbo la Morogoro kusini na nafasi yake kuchukuliwa na Mbena na
aliyekuwa mbunge wa mikumi Abdusalam Ameir akiangushwa jimbo la Mikumi
na nafasi hiyo kuchukuliwa na Jonas Estomih nkya.Chanzo http://www.eatv.tv/news
Comments