Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa wanaozania kuwa CCM ni chama
cha mchezo watakiona cha mtemakuni katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka
huu.
Dk.
Kikwete ambaye pia ni rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania, amesema
hayo leo Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa katika uchaguzi huo CCM
watafunga magoli huku upinzani wakiishia kutazama tu.
Dk. Kikwete ambaye alikuwa akimkaribisha mgombea wa CCM Dk. John
Pombe Magufuli mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urasi kutoka Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, amesema CCM haiwezi kumdharau adui yoyote kwa kuwa
hii ni vita.
Akiongea katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Abdulrahman
Kinana amesema kuwa katika uchaguzi huu CCM kinapambana na makapi yake
hivyo hakitapata tabu kushinda kauli ambayo inamlenga mgombe wa Chadema
Mhe. Edward Lowassa ambaye amejiondoa CCM.
Comments