Nahodha wa timu ya Twiga Stars, Sophia Mwasikili
amesema, wanaamini watafanya vizuri na kuibuka na ushindi katika
mashindano ya All African Games yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi
Septemba nne mwaka huu nchini Congo Brazzaville.
Akizungumza
na East Africa Radio, Sophia amesema, wanapokea mazoezi wanayopewa na
yanazidi kuwapa hamasa na kuwaonyesha kuwango chao ili kuweza kufanya
mabadiliko zaidi pale wanapoona kunamapungufu.
Sophia amesema, licha ya kukosa mechi nyingi za kirafiki lakini Kocha
Kaijage anawajenga kisaikolojia na kila mchezaji anahari ya kujifunza
zaidi kile kocha anachofundisha na wanaamini mechi za kirafiki
wanazocheza mechi nja wanaume zitazawasaidia kuweza kufika mbali zaidi
katika soka.
Sophia amewataka watanzania kuwa na imani kama waliyokuwa nayo kwani
wanaweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya All African Games.
Comments