Na Hamida Hassan
Mastaa
wengi wamekuwa hawadumu kwenye ndoa zao na wengine kwenye uhusiano wao
wa kimapenzi. Ukijaribu kumuuliza kijana yeyote mwenye nia ya kuoa
atakuambia bora aoe mwanamke wa kawaida kuliko staa.Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Si
suala la kuoa tu, hata kwenye mapenzi ya kawaida ni wachache
wanaoanzisha uhusiano na mastaa wakiwa na ndoto za kudumu kwa muda
mrefu. Ukiona kijana ‘anamsalandia’ staa ujue ni ili amuonje tu kisha
amtose.
Pia
ukifuatilia utagundua kuwa, mwanamke wa kawaida akitokea kumpenda staa
wa kiume, anatafuta ile sifa ya kuwa naye lakini anajua hawezi kudumu
naye.Kutokana na hilo sasa, makala haya yanajaribu kukupa kwa ufupi
sababu 10 ambazo zinawafanya mastaa wengi wa kike kutodumu kwenye ndoa.
Tamaa
Hili
lipo sana kwa mastaa wa kike. Baadhi yao wana tamaa ya kuwa na maisha
f’lani ili waonekane nao wamo wakati uwezo haupo. Matokeo yake sasa
akiolewa na mwanaume ambaye hana kitu, akimpata wa pembeni ‘pedeshee’ wa
kumtunza, kwa tamaa zao hujikuta wakisaliti.
Unakuta
msichana kwa kuwa ni staa, anataka awe na gari zuri, abadili nguo kila
siku, simu kali na vitu vingine vya thamani wakati pesa hana na mume
naye ni kapuku. Hapo ndipo wengi huamua kuchepuka na matokeo yake sasa
hajali tena ndoa.
Ustaa mwingi
Mastaa
wengi wakishajitambua kuwa wao maarufu, basi hata kwa wapenzi wao
wanaleta zile nyodo za ustaa. Wanasahau kuwa hata rais anapokuwa na
mkewe humnyenyekea kama mke na mambo mengine kuendelea.
Utakuta staa anataka kuonesha ustaa wake kwa mumewe, yaani anataka mume awe chini yeye awe juu kisa tu anatikisa jiji.
Halima Yahaya ‘Davina.
Unyenyekevu
katika mapenzi unakuwa haupo, eti anajipa imani kwamba hata akiachwa
kwa kuwa anapapatikiwa na wanaume wengine kutokana na ustaa wake,
hatakosa wa kumchukua. Hiyo ni dhana potofu!
Uvivu, kupenda kulala…
Baadhi
ya mastaa hata wakiolewa wanashindwa kuvaa joho la ‘mke wa mtu’.
Wanapenda kukaa tu na kuletewa kila kitu nyumbani. Akicheza muvi moja na
kujulikana basi anaona dunia ndiyo yake, hakumbuki kutafuta kazi ya
uhakika.
Usiku atapenda atoke, mchana ni mtu wa kulala tu kisa kachoka. Ni mwanaume wa aina gani atakayemvumilia?
Starehe kwa sana
Mke
wa mtu hata kama anastahili kustarehe siku mojamoja, lakini baadhi ya
mastaa walioingia kwenye ndoa huona wao starehe lazima ichukue sehemu
kubwa ya maisha yao. Atalazimisha kila siku watoke na hata kama mume
atakuwa si mtu wa kuendekeza mambo hayo, yeye ataomba awe anaenda na
mastaa wenzake, akikataliwa inakuwa tatizo.
Hawajitambui
Mastaa
wengi wanakosa elimu ya kujitambua. Ndiyo maana wengi wanaitwa
malimbukeni. Unakuta staa amepata mume mzuri tu lakini yeye anashindwa
kujitambua kuwa yeye ni mke wa mtu asiyestahili kuingiza ustaa wake
kwenye maisha yake ya nyumbani.
Ndoa fasheni
Jaribu
kuchunguza utagundua kuwa, mastaa wengi wanaolewa kama fasheni.
Utamkuta staa wa kike anasema wazi kwamba, amechangia wengi sana hivyo
na yeye anataka kuchangiwa hivyo analazimisha kuolewa.
Wanaoolewa
kwa sababu hiyo ni wale ambao hata ndoa zao zikivunjika hawaoni hatari,
wanaona ni sawa tu kwa sababu angalau wameonja ndoa!
Judith Wambura ‘Jide’.
Uvumilivu wa shida
Mara nyingi watu wanapooana hukubaliana kuishi pamoja kwa shida na raha. Mastaa wengi hawataki shida, wao wanataka raha tu.
Matokeo
yake sasa ukiona mambo yanaenda kombo, ni wachache sana wanaoweza
kuvumilia shida. Wengi wataanza visa na hatimaye wataomba talaka au
kuamua kutoka kwenye ndoa!
Dhana potofu
dhidi yao
Mastaa
wengi wanaonekana si watu wa kuolewa. Sasa anapotokea mwanaume wa
kumuoa staa, hata kwenye mambo ya kawaida ataona anafanyiwa hivyo kwa
sababu ya ustaa.Matokeo yake sasa, hata kama staa huyo atajitahidi ili
adumu kwenye ndoa yake atashangaa ile damu ya ustaa inamtesa.
Wanakosa staha
Mke
kama mke lazima awe na staha, kitu ambacho baadhi ya mastaa wanakikosa.
Utakuta staa kaolewa lakini ana marafiki wengi wa kiume na anataka mume
wake asihoji juu ya urafiki wao.Kama ni msanii akiwa lokesheni,
afanyiwe lolote na wanaume, avae nguo hata za utupu kisa eti anaigiza.
Mbaya zaidi si lokesheni, hata nje ya fani wanataka kuishi kisanii.
Jack Patrick.
Wako tayari kuachika
Mastaa
wengi wa kike wakiolewa, wanakaa mkao wa kuachika wakati wowote. Ni
wachache wanaofanya jitihada za kutunza ndoa zao. Yaani wanatembea
kwenye ile dhana potofu kwamba staa hawezi kudumu kwenye ndoa.
Sababu hizo hapo juu na nyinginezo ndizo zilizosababisha ndoa za mastaa kama vile Nuru Na.Inatoka http://matukiouk.blogspot.com/
Comments