Skip to main content

Dk Slaa: Niko salama, nitazungumza muda ukifika


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Japhary Michael (kushoto) na viongozi wengine wa chama hicho walipomtembelea Slaa nyumani kwake Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Japhary Michael (kushoto) na viongozi wengine wa chama hicho walipomtembelea Slaa nyumani kwake Dar es Salaam jana.
Siku tatu baada ya Baraza Kuu la Chadema kuridhia kumpumzisha kwa muda Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa baada ya kutofautiana na Kamati Kuu kwa kumkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kiongozi huyo amesema yupo salama na wakati mwafaka ukifika atazungumza ya moyoni.
Akizungumza kwa mara ya kwanza na gazeti hili tangu Chadema imkaribishe Lowassa na hatimaye kumpitisha kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa,
Dk Slaa alisema amekuwa akisikia mengi yakisemwa juu yake lakini yote yamekuwa yakimchekesha tu.
Hakuhudhuria vikao muhimu vya chama hicho na vile vya Ukawa, vikiwamo; wakati Lowassa akitambulishwa rasmi, akichukua fomu, kikao cha Baraza Kuu na juzi Mkutano Mkuu na hakuwa akipatikana kwa simu yake ya mkononi.
Wakati kimya kikitawala juu ya hatima yake, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuwa amejivua uanachama Chadema.
Lakini jana alisema ‘Naangalia mambo mengi yanayoendelea kwenye mitandao halafu ninacheka tu, usifikiri sifuatilii, nafuatilia kinachoendelea na ninabaki nikicheka.’
Kuhusu hatima yake kisiasa na madai ya kujiuzulu uanachama ndani ya Chadema,
alisema hawezi kuzungumza lolote kwa sasa na atafanya hivyo wakati mwafaka ukifika.
‘Usijali wakati wangu wa kuzungumza ukifika nitasema tu, sasa hivi nawaachia mzungumze, lakini nitazungumza,’alisema.
Kadhalika, alipoulizwa kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa maisha yake yapo hatarini kwa kuwa anatishwa, Dk Slaa alisema hata hilo pia atalizungumzia wakati mwafaka ukifika.
‘Ndiyo hayohayo ninayosema, wala msijali nitazungumza wakati ukifika,’ alisema na kusisitiza: ‘Nipo salama.’
Dk Slaa alisema kwa sasa yupo mapumzikoni nje ya jiji la Dar es Salaam ingawa hakutaka kueleza ni eneo gani.
Juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifafanua tofauti iliyojitokeza kati ya Kamati Kuu ya Chadema na Dk Slaa wakati wa mchakato wa kumpokea Lowassa.
Katika mkutano huo wa Baraza Kuu la Chadema, Mbowe alisema wamekubaliana katibu mkuu huyo apumzike kwa muda… ‘Nina hakika kwa tabia na hulka za Dk Slaa… kwa sababu anajua
tunampenda na yeye anakipenda chama hiki, tunamwombea kwa Mungu ampe nguvu na ujasiri wa kuona kwamba kauli ya wengi ni kauli ya Mungu.’
Ndesamburo na siri nzito
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na makada wengine wa Chadema, jana walikwenda kuonana na Dk Slaa nyumbani kwake na kufanya naye kikao cha faragha.
Picha zilizomuonyesha Ndesamburo akiwa na Dk Slaa na makada wengine akiwamo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Jaffar Michael,
zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii jana na kuibua mijadala.
Baadhi ya waliochangia mijadala hiyo walidokeza kuwa huenda Ndesamburo anayeheshimika ndani ya chama hicho alikwenda kujaribu kusawazisha hali ya mambo.
Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alikiri kuwa picha hizo ni halisi, baadhi zilipigwa juzi na nyingine jana mchana, lakini hakutaka kuingia undani wa mkutano wa wanasiasa hao.
Ndesamburo alithibitisha kukutana na Dk Slaa: ‘Ni kweli tulikwenda, kwani kuna tatizo gani? Si mzee mwenzangu?
Halafu bado ni mwanachama wetu, hajatoka Chadema, hivyo tuna kila haki ya kwenda kumsalimia.’
Alipoulizwa kama alikwenda kumsihi Dk Slaa arejee kuendesha mapambano ya kuing’oa CCM, Ndesamburo alisisitiza kuwa walikwenda kumsalimia.
Michael alipoulizwa nia ya safari hiyo alijibu kwa kuuliza; ‘Dk Slaa ni katibu mkuu wetu kwani tunazuiwa kwenda kumsalimia?’
Dk Slaa aligombea urais mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili baada ya Rais Jakaya Kikwete na ndiye aliyekuwa akitajwa kuwania tena nafasi hiyo kupitia Chadema na Ukawa kabla ya ‘kubadili gia angani’ na kumteua Lowassa.
Chanzo:Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...