Tume ya
Ulaya imetangaza Jumatatu wiki hii kutoa Euro bilioni 2.4 kwa nchi
zinazowapokea wahamiaji. Msaada huu kwa nchi wanachama 19 umepangwa kwa
kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020.
Kama
tangazo hili sio majibu ya moja kwa moja kwa ombi la msaada lililotolewa
wiki iliyopita na Ugiriki pamoja na Italia, ni hatua ya kuzisaidia nchi
zinazokabiliana na ongezeka kubwa la watu wanaotafuta hifadhi ya
ukimbizi.
Kwa
tangazo hili, Tume ya Ulaya imehalalisha mipango 23 ya kitaifa katika
suala la usimamizi wa ongezeko la uhamiaji. Fedha hizi, ziliyopangwa kwa
kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020, zitasaidia nchi nyingi zilioathirika
na ongezeko la watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi. Italia itapewa Euro
milioni 560, na Ugiriki itapewaEuro milioni 473. Lakini nchi nyingine
wanachama ambazo zinakabiliwa na hali hii pia na tatizo hili pia
zitanufaika na fedha hizo za Ulaya. Uhispania, Sweden au Bulgaria ni
miongoni mwa nchi hizo.CHANZO:RFI KISWAHILI
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON
Zoezi la
kutolewa kwa fedha hizo na Tume ya Ulaya lilianza Machi na linatarajiwa
kuendelea katika majuma yajayo. Njia hizi, zilizotokana na taratibu
mbili za Ulaya, zina malengo tofauti. Lengo la wanza unakuja kusaidia
nchi wanachama ili kuboresha uwezo wao wa mapokezi na ushirikiano kwa
watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi. Lengo la pili linatilia mkazo
umakini juu ya masuala ya usalama, ikiwa ni pamoja na kuboresha
usimamizi na ufuatiliaji wa mipaka. Lakini fedha hizi pia zitasaidia
kupambana dhidi ya ugaidi na aina zote za usalama barabarani.
Kwa
tangazo hili, Tume ya Ulaya imsema inataka kuendesha kazi hii kwa moyo
wa mshikamano. Moja ya njia ya kuzikumbusha nchi wanachama kuzingatia
majukumu yao.
Comments