Spurs imefanikiwa kumsajili winga mshambuliaji aliyekuwa katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani Son Heung-Min ambaye
ni raia wa Korea Kusini kwa mkataba wa miaka 5 baada ya kumfanyia
vipimo vya afya na kufuzu. Dau la pound milioni 21.9 lilitosha
kuishawishi klabu ya Bayer Leverkusen kumuachia winga huyo.
Tottenham Hotspur inamleta Son Heung-Min aliyeifungia Bayer Leverkusen magoli 21 katika mechi 58 za Bundesliga ili aje kushirikiana na Harry Kane ambaye ni mshambuliaji wa kati tegemeo kwa klabu ya Tottenham Hotspur.
Comments