Mwanariadha Oscar Pistorius.
Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Oscar Pistorius akiwa mahakamani wakati wa kesi yake.
Mwanariadha
mahiri wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatarajiwa kuachiwa
Ijumaa hii baada ya kuonyesha tabia nzuri akiwa gerezani. Pistorius
alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka uliopita kwa kosa la
kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika usiku wa Siku ya Wapendanao
'Valentine's Day'.(P.T)
Pistorius
ametumikia kifungo cha miezi 10 pekee gerezani kati ya miaka mitano
aliyohukumiwa. Baada ya kuachiwa, Pistorius anatarajiwa kuwa akitumikia
muda wake uliobaki akiwa katika kifungo cha nje.
Wakati
akitoa hukumu ya staa huyo, Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa kiongozi
wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa Pistorius
alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp alipompiga risasi nyumbani
kwake akidhani kuwa ni mwizi.
Comments