Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Eliamani Mbise amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msajili wa Mahakama ya Rufani Francis Mutungi imesema Jaji Mbise amefariki majira ya saa nne na nusu tarehe 29/7/2010 .
Taarifa hiyo imesemakuwa taratibu za mipango ya Mazishi ambayo yatafanyika Arusha itatolewa baadae baada ya utawala kuwasiliana na ndugu wa marehemu.
Aidha Bwana Mutungi amesema msiba umewekwa kwa muda nyumbani alipokuwa akiishi marehemu Mikocheni kwenye nyumba za viongozi wa Serikali.
Marehemu Mbise alikuwa akifanya kazi katika kituo cha kazi cha Mahakama kuu ya Tanzania .

Comments