Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WANACHAMA wa klabu ya Yanga kwa kauli moja wamekubaliana kumrejesha madarakani, Mwenyekiti wao Yussuf Mehboob Manji katika mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam leo. Pamoja na kumrejesha Maji aliyejiuzulu Mei mwaka jana, wanachama hao wameunda Kamati ya watu tisa chini ya Rais wa zamani wa klabu, Tarimba Abbas kusimamia usajili na mambo mengine muhimu ya klabu kwa sasa. Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mkutano huo, Kaimu Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe kufanyika kwa uchaguzi wa kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu ndani ya miezi miwili pia linafanyiwa kazi. Mkwasa pia amesema kwamba wameridhia mwongozo wa mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu kwa kuingia kwenye soko la hisa na kwamba mchakato wa zoezi hilo unashughulikiwa na Wakili maarufu, Alex Mgongolwa....