Shirika la Afya Duniani, WHO limetoa takwimu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Takwimu
hizo zinazihusu nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia tu ambapo
taarifa zinasema kumekuwa na wagonjwa 23 218 na vifo 9365.
Mchanganuo
wa takwimu hizo unaonyesha kuwa Sierra Leone imekuwa na wagonjwa 11
103, na vifo vya watu 3408, Liberia - wagonjwa 9007, vifo 3900 na Guinea
- wagonjwa 3108 na vifo vya watu 2057.
Takwimu hizo ni mpaka tarehe 15 Februari kwa nchi za Sierra Leone na Guinea, na Liberia ni mpaka tarehe 12 Februari.
Pia Uingereza ilikuwa na mgonjwa mmoja bila kifo
Takwimu
kwa ajili ya Senegal, Nigeria, Hispania, Marekani na Mali
zimeondolewa.Nchi hizo haziko katika karantini ya ugonjwa wa Ebola.CHANZO:BBC
Comments