Benki zinazoshughulikia uamisho wa pesa kutoka katika familia za
Wasomali wanaoishi Marekani kutumwa Afrika Mashariki zimefungwa kutokana
na kitisho cha pesa hizo kusambazwa kwa wanamgambo wa Al Shabab.
Wafanyabiashara wa benki kuu California hushughulikia hadi asilimia
80 ya uhamisho kutoka Marekani wenye thamani ya dola milioni 200 kwa
mwaka.
Wakuu wa mabenki hayo wamesema hakuna uwezekano wa kuendelea na
uamisho wa fedha kutokana na kugundulika kwa kanuni mpya chafu ya
matumizi ya fedha hizo.
Wajumbe kutoka Marekani wamesema ili litakuwa ni janga kwa Wasomalia wanaoishi Afrika Mashariki.
Kuna wasiwasi kwamba baadhi ya fedha zinazotumwa zinaingia mikononi mwa wanamgambo wa Al shabab.
Comments