Watu zaidi ya 70 wameuwa katika wilaya iliyo nje kidogo na mji wa
Damascus kwenye shambulizi la anga lililotekelezwa na jeshi la Syria
baada ya waasi kushambulia ngome inayodhibitiwa na jeshi la hilo kwa
kutumia rocketi.
Wachunguzi wa haki za binadamu wanaofatilia vurugu zinazoendelea
Syria wamesema kwamba katika shambulizi hilo watoto 12 na wapiganaji 11
ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha.
Hivi karibuni vifo vya mashambulizi ya kutoka angani vimeongezeka nchini Syria.
Comments